Wednesday, 28 August 2013

KEJO COMMUNITY KUANZISHA LIGI YA NGO'MBE

Kikundi cha kijamii chenye makazi yake keko mowlem cha panga kuanzisha ligi ya Ngo'mbe kwa mshindi wa kwanza na mbuzi kwa mshindi wa pili,Ligi hiyo itakayoanza keko juu na kumalizikia Uwanja wa sigara maarufu kama TCC.ufunguzi wa mashindano hayo yatafanywa na Diwani wa kata ya keko Mh.Francis Mtawa na kufungwa na Mbunge wa temeke Mh.Abbas Zuberi Mtemvu.Timu 16 zimethibitisha kushiriki kwa ligi hiyo ambayo itatimua vumbi tarehe 7/9/2013 panapo majaliwa

KEJO YATOKA SARE YA 3-3 NA POLICE BAGAMOYO

                                            kikosi
                                          kikosi
                                         Safari ilianzia hapa

                                           kikosi
                                             kikosi
                                            kikosi
                                             kikosi

                                              Half time



                                             Foward Jailo mwambande alikuwa mwiba kwa police alifunga magoli mawili

                                                    Kipa wa police bagamoyo

                                                     Mchezo ukiendelea

                                                     Mchezo ukiendelea
                                                     Police akibanwa na msuli

                                                     Mchezo ukiendelea

                                         Mchezaji wa polisi bagamoyo akifuatilia mechi inavyokwenda

                                                      Akifurahia mchezo unavyokwenda


                                 mchezaji wa polisi akiwa amelala kwa kupata maumivu


                                                    Kocha wa kikosi cha polisi bagamoyo






                                                Kikosi cha polisi upande wa bagamoyo waliovalia jezi nyeupe
                                        Katibu ndani ya police Mess kama kawaida yetu kejo

                                          Viongozi wakifanya yao
















Wednesday, 14 August 2013

TUKUMBUSHANE BAHADHI YA MATUKIO YALIYOPITA YA KEJO

 Tukiwa cuo kikuu cha Dar es Salaam tyari kwa ajili ya mechi
 Moja ya shughuli za kijamii zilizofanyw ana kejo hapa ni ujenzi wa Daraja la kwa Bibi Mode hili ni moja kati ya madaraja matatu yaliyojengwa na kejo katika mfrejei wa molemo kurahisisha kuvuka kwa watu wazima na wanafunzi wa shule ya msingi Magurumbasi na Sekondari ya Keko kutwa
 Ostadh Daudi akifuturu wakati mwezi mtukufu pindi blog ya kejo ilipomtmebelea
 pia masiahara yapo katika kundi letu hpa Jairo Mwambande akiwa na Godi Sungura wakati wa mechi tuliyocheza ubongo msewe
Pia ujasiliamali ni sehemu yetu hpa mkongwe sadick akipaka polish moja ya vitanda vya wateja wake

Tuesday, 13 August 2013

HATIMAYE KEJO COMMUNITY YAPATA VIONGOZI WAPYA

Baada ya msuguano wa muda mrefu kikundi cha kijamii chenye maskani yake huko keko hatimaye kimepata uongozi mpya habari hizi zenye ukweli zimepatikana kutoka kwa moja ya viongozi waliowai kukaimu nafasi ya mwenyekiti na alipoulizwa na mwandishi wetu kuhusu uongozi uliochaguliwa tarehe 10/8/2013 maeneo ya DDC keko amesema ana imani kubwa saba na uongozi uliopitishwa na wanachama wenyewe tunawaombea watuendeshe vizuri kwa kipindi chao chote.
Nae mwenyekiti wapya pamoja na katibu wake wameiakikishia wanachama wa KEJO COMMUNITY watafanya mambo makubwa waliyoyapanga."Kwa sasa kikundi chetu kina uongozi sabiti na hakitaki mchezo katika mambo ambayo hayatakuwa mazuri kwao na kikundi kwa ujumla"KEJO COMMUNITY sasa inatambulika kisheria.Hapo chini ndio nguzo iliyochaguliwa na wanachama

MWENYEKITI
Neston Adam Kenan

M/MWENYEKITI
Robert Paul Mlowoka

KATIBU
Fabian Mtono

M/KATIBU
Benjamini O.Msegere

MAKAMANDA
1.Jafari Rajabu
2.Shadrack Mwandumusya

KAMATI KUU TENDAJI
1.Jailo Nelson Mwambande
2.Eria Mwakipande
3.Daimon Alexander

MTUNZAHAZINA
1.Bony Boaz

M/MTUNZAHAZINA
Jailo Nelson Mwambande

AFISA HABARI
1.Humphrey Shao
2.Thania

Hiyo ndio safu ya uongozi wa KEJO COMMUNITY yenye kauli mbiu "PAMOJA TUTAFIKA"
                                     
  MUNGU IBARIKI KEKO,MUNGU IBARIKI MOWLEM,MUNGU IBARIKI KEJO COMMUNITY

Wednesday, 7 August 2013

WAKALI WA STORY MPO

Mpendwa,

Siku moja punda wa mkulima alianguka ndani ya kisima. Mnyama huyo alipiga kelele kinyonge kwa masaa kadhaa wakati mkulima akijaribu kufikiri nini cha kufanya.
Hatimaye, aliamua kwakuwa punda wake alikuwa mzee, na pia kisima hicho kilihitaji kufunikwa juu, Akaona hapakuwa na haja ya kumtoa.

Akaita majirani zake wote waje kumsaidia. Wao wote wakachukua makoleo na kuanza kuchota taka kwa koleo na kuzitupia ndani ya kisima.
Mara ya kwanza, punda aligundua nini kilikuwa kinatokea akapiga kelele kwa nguvu. Basi, ikawashanganza wale watu punda aliponyamaza ghafla!
Baada ya kutupa taka kadhaa kwenye hicho kisima. Huyo mkulima alishangazwa na kile alichokiona. Kwamba kila koleo la taka lililorushwa juu ya mgongo wa punda, punda alikuwa akifanya kitu cha kushangaza. Alikuwa akijitikisa ili taka zimwagike chini huku akipiga hatua moja kuja juu.

Kadri mkulima na majirani walivyoendelea kutupa uchafu kwa koleo juu ya punda yule, alizidi kutikisa mgongo wake na kupiga hatua moja kuja juu. Muda mfupi baadae, kila mtu alishangaa jinsi punda alivyozidi kutokeza ndani ya kisima na kuja juu.



FUNZO:
Maisha yatakutupia kila aina ya uchafu. Ili utoke nje ya kisima wahitaji kujitikisa na kuchukua hatua moja juu. Kila tatizo ulilonalo, ni jiwe la kukuwezesha kukanyaga na kupiga hatua kuja juu. Tunaweza kutoka nje ya kisima kirefu kwa kuongeza bidii ya kupiga hatua moja kuja juu bila kuacha na kutokata tamaa kamwe. Tikisa itikisa uchafu mbali na kuchukua hatua kuja juu.
Kumbuka kanuni 5 rahisi ili uwe na furaha:
1. Weka huru moyo wako mbali na chuki - Samehe.

2. Weka huru akili yako mbali na wasiwasi - Wengi hushindwa kabisa kipengele hiki.

3.Tosheka / rizika na ulichonacho.

4. Toa zaidi.

5. Tarajia vichache kutoka kwa watu lakini zaidi kutoka kwako mwenyewe.

Una uchaguzi wa aina mbili ...
i) Tabasamu na funga ujumbe huu,
ii) au tuma ujumbe huu kwa mtu mwingine ili ashiriki somo hili